Mercedes Benz Club Kenya wagusa mioyo ya wakaaji Taita Taveta

113 150

Juhudi za wizara ya elimu nchini kuboresha sekta hiyo zilipigwa jeki kaunti ya Taita Taveta baada ya Mercedes Benz Club Kenya (MBCK) kuanzisha mradi wenye tija inayolenga kurejesha hadhi ya mtoto wa kike kwenye jamii sawia na kuboresha matokeo kwa kuleta suluhu la kudumu kwa changamoto zilizopo.

MBCK ambao walizuru shule ya msingi ya Mambura eneo bunge la Mwatate na kupeana taraklishi, mashine za kuchapisha mitihani ya majaribio, chakula na sodo walizindua mradi wa ujenzi wa choo cha kisasa ili kufidia kile kinachotajwa kama haibu shuleni humo kwani waalimu, wanafunzi na jamii zinazopakana na shule hiyo wamekua wakishiriki choo kimoja.

Kwasasa wanayataka mashirika mbalimbali ya kijamii, wafanyibiashara na wadau wa sekta mbalimbali kujitolea na kuunga mkono juhudi walizoanzisha kwa lengo la kuinua sekta ya elimu kote nchini.

Licha ya changamoto hizo, shule hiyo iliandikisha alama 270 kwenye matokeo ya mtihani wa kitaifa KCPE 2021 na kufanikiwa kupeleka watoto 3 shule za kitaifa.