Raila amteua Karua 

160 150

Kinara wa Narc-Kenya Bi. Martha Karua ndie mgombea mwenza wa Raila Odinga. Karua aliyewai kua mbunge wa Gichugu na pia waziri katika serikali zilizotangulia anauletea mrengo wa Azimio tajriba yake ya muda mrefu kwenye fani ya siasa ikiwemo msimamo wake dhabiti kwenye maswala yanayohusiana na uongozi wa taifa.

Kwenye wasifu wake wakati wa kutoa tangazo hilo mapema leo katika ukumbi wa KICC, Mgombea urais wa Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga amemtaja Karua kama mtetezi wa haki za wakenya na kua atahudumu kama waziri wa sheria, jukumu kuu likiwa kupigania katiba.

Miongoni mwa watakaounda serikali ya Azimio La Umoja One kenya ni pamoja na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka (Mkuu wa mawaziri), Hassan Joho (waziri wa ardhi), Peter Munya (waziri wa kilimo), Wycliff Oparanya (waziri hazia kuu), Kenneth Marende (Spika wa bunge la seniti)